Monday, September 17, 2012

NI MUDA WA KUBADILISHA MIFUMO ISIYO NA FAIDA KWETU,TUENDELEZE MPIRA,.................VODACOM PREMIER LEAGUE 2012/13

Ni msimu mwingine wa ligi ya Vodacom ambao umechukua sura mpya kulinganisha na miaka mingine,kwanza package ya zawadi ikiongezeka kufikia millioni 70 kwa bingwa na milllioni 45 kwa mshindi wa pili na millioni 30 kwa mshindi wa tatu,lakini vilevile ligi ipo mikononi kwa taasisi binafsi maarufu kama kamati ya ligi ambayo wadau wamekuwa wakiipigia kelele,kwa mtazamo wangu ni hatua nzuri lakini kama hiyo kamati itakuwa na watu ambao wana kiu ya maendeleo ya soka nchini,je ni kweli ligi yetu itaboreka baada ya kamati kuchukua majukumu ya kusimamia ligi? Mimi mwandishi wa hii blogi na wewe mpendwa msomaji hatujui,tusubiri tuone.
Lakini wakati hii kamati ikichukua mamlaka ya kuiongoza ligi ya vodacom nchini,kuna mkataba ambao kampuni ya simu za mikononi imeingia,upande wa kwanza ni kampuni na upande wa pili ni shirikisho letu TFF au kamati ya ligi ambayo inachukua majukumu,je ni nani anayestahili kuingia na vodacom mkataba,na umesainiwa wapi na lini,hayo ni maswali ambayo mkurugenzi wa kamati ya ligi na rais wa TFF wanayo majibu,sawa moja ya madhumuni ya kamati ya ligi ni kuhahkikisha kila timu inaweza kushindana katika ligi hasa kwa timu ndogo ambazo kiuchumi hawako vizuri,kwa sababu kuna vipengele vinavyofanya ugawanywaji wa mapato uwe na uwiano kiasi fulani.
Kwa miaka kadhaa sasa ligi yetu imekuwa ikiendeshwa kwa mizengwe ya hapa na pale,kila mwaka kubadilika kwa ratiba bila sababu za msingi,kuongeza siku za usajili bila sababu,kuingiliana mamlaka baina ya kamati za TFF,ndio maana hata TFF hawakua tayari kuiachia ligi kwa kampuni binafsi ingawa mimi  mwenyewe siko upande  wa hiyo kamati hadi nione kweli tulikuwa sahahi kulilia kamati,kwa kuanza waanze na njia sahihi za kumapata mdhamini na siyo kujikomba au kupelekwapelekwa na mdhamini mmoja anbaye masharti yake na package anayotoa si sawa,masharti yamekuwa mengi mno,nashukuru katika huu mkataba ambao hatujui uliposainiwa badge ya mdhamini itakaa mkononi na si kifuani,atakeyakaa kifuani ni yule mdhamini wa timu,hebu tuanzie na hapa.

No comments: