Siku ishirini na kadhaa zilizopita nikiwa natembea kwa kasi,sio kasi sana maana naogopa nitatoka jasho sana kwa sababu naelekea ofisini,ni mtaa maarufu hapa jijini Dar es salaam,ni samora,mara kuna kitu kinanifanya nipunguze kasi,si kingine ni habari za mchezo maarufu duniani na unaopendwa na watu wengi duniani kutokana na ka utafiti kangu nilikokafanya,ni habari zilizoojuu ya kila ukurasa wa magazeti mengi ya michezo.'''Ni habari za usajili wa timu za ligi kuu Tanzania maarufu kama ligi ya VODACOM,zimepambwa ili tu kuvutia soko la uuuzaji wa hayo magazeti,nashawishika kununua,natoa 500 yangu mfukoni nanunua mojawapo.Napata hisia kubwa ninaposoma lile gazeti.
Hisia ninayoipata ni kwamba nikae tayari kuangalia ligi ya ushindani ya nchini Tanzania kutokana na usajili sio nilivyoona hao watu waliosajiliwa wakicheza ila kwa maelezo ya waandishi wa habari wenye taaluma zao na waliosomea kwa miaka kadhaa,napata shauku ya kuhudhuria angalau mechi kadhaa ili nijue je ni usajili wa kweli hasa wa hao wanaoitwa ma-PRO.
Ni ma-PRO kweli ukilinganisha na mishahara wanaayoipata asilimia kubwa ya wazawa wetu,''professional player'' ni mchezaji anayepata kipato kinachozidi matumizi yake kwa mwezi kutokana na maelezo ya FIFA,je kama kuna mchezaji nchi hii anapokea kiasi cha dola 3500 kwa mwezi si professional,haizidi yale matumizi muhimu ya mtu kwa nchi yetu? mimi na wewetujiulize?
Hao tunaowaita ma-PRO wanakidhi mahitaji ya timu pindi wanapoanza kuzitumikia timu zao,kwa mfumo wa ligi zetu afrika mashariki na kati mchezaji haitaji mda mrefu sana kuzoea mazingira ili kuweza kuitumikia klabu yake kwa ufanisi,lakini swali la kujiuliza kwenye watu millioni tumeshindwa kuzalisha vipaji na kuanza kupigana vikumbo katika usajili wa hao tunaodai wana uwezo kuliko sisi.
Baada ya hayo yote kinachonishangaza katika usajili hapa Tanzania je kuna watu maalium wanaohusika na usajili au ni watu tu kwenye timu kwa sababu wao ni wasaidiaji wa timu pale zinapoyumba kiuchumi,je timu zinasajili kwa matakwa ya kocha,jibu ni hapana,mwisho wa siku tunamuona kocha afanyi kazi yake,namnukuu mmoja wa makocha wa timu kongwe nchini yenye maskani yake mtaa wa msimbazi'''SIMBA SPORTS CLUB''''Mchezaji niliyempendekeza ni mmoja tu,MRISHO NGASSA,hawa wengine wamesajiliwa na viongozi na kama nitaendelea kuwepo sitoruhusu huu utaratibu,ndio maana nawaangalia kama wananifaa nabaki nao na wasionafaa nawaacha,klabu ya simba imeingia hasara sana msimu huu kutokana na uzembe wa kusajili bila matakwa ya kocha matokeo yake timu bado ina mapungufu ingawa wenyewe wanaiona ipo sawa,na hii tabia hata kwa ''''DAR YOUNG AFRICANS FC'''sikumbuki lini hizi timu zilikuwa na watu wanaohusika na kufanya uchunguzi juu watu ambao wanataka kuwasajili,mwisho ni lawama kwa benchi la ufundi wa timu wakati mashabiki walikuwa wanayajua yote hayo waliyafumbia macho.
Chanzo cha haya yote TFF imeshindwa kutekeleza azimio lake la kila timu iwe na timu ya vijana,ukiuliza udhamini lakini naamini fedha za goal project za FIFA ambazo sisi hatuzitumii ipasavyo na shirikisho lenyewe lina vyanzo vingi vya fedha na sijui kwanini wanashindwa kufanya haya yote,je kwanini twasiweke kipengele ambacho mdhamini wa ligi kuu awe na uwezo kwa asilimia flani kudhamini ligi ya vijana angalau hata kwa asilimia 40.au kampuni ya coca-cola ambayo kila mwaka inadhamini ligi za vijana mimi bado naamini TFF wanaweza wakaka nao mezani ili waweze kusaidia vijana ilimwisho wa siku zile dola 3500 ziende kwa mzawa.
Hata kama viongozi wakipendekeza usajili na timu ikawa vizuri kutokana na usajili bado si sahihi,ndio maana kila mwaka Simba na Yanga zinakuwa na utata katika timu zao kwa sababu viongozi wa timu hizi kuna mwaka wanapatia na kuna mwaka wanakosea katika usajili jambo ambalo kama wangemshirikisha mwalimu basi makosa yangekuwa kidogo kwa sababu si kila usajili atakaofanya mwalimu utafikia malengo bali utapunguza makosa kama ungefanywa na viongozi,umefika wakati wa viongozi kuendesha vilabu kwa mifumo inayotakiwa ikiwezekana kuwe na ''''chief scout'''katika kila kilabu ili makosa katika usajili yasiwe mengi............nakala imeandikwa na mmiliki wa blogi hii '''JURGEN,EMMANUEL''''
No comments:
Post a Comment