NI TP MAZEMBE VS ESPERANCE NUSU FAINALI ORANGE CHAMPIONS LEAGUE
TOUT
Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) sasa itamenyana na
Esperance ya Tunisia katika Nusu Fainali ya Mabingwa Afrika, kufuatia kuchapwa
bao 1-0 na Berekum Chelsea ya Ghana usiku huu kwenye Uwanja wa Ohene Djan
Sports mjini Accra.
Kwa matokeo
hayo ya Mazembe kutulizwa kwa bao pekee la J. Darko-Opoku dakika ya 80, akiunganisha
pasi ya I. Issaka, sasa imemaliza kama mshindi wa pili kwenye Kundi B kwa
pointi zake 10 na Aly Ahly iliyotoka sare ya 1-1 na Zamalek imekuwa kinara wa
kundi hilo kwa pointi zake 11.
Mazembe ya Lubumbashi,
yenye washambuliaji wawili wa Kitanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel
Ulimwengu ilitaka kushinda mechi hiyo ili kuongoza Kundi ikwepe kucheza na Watunisia,
lakini imeshindikana.
Katika mchezo
wa leo, Samatta alicheza dakika zote 90, wakati Ulimwengu aliingia kuchukua
nafasi ya D. Kanda dakika ya 76.
Mohamed
Ibrahim alitangulia kuifungia Zamalek dakika ya 43 kwenye Uwanja wa Jeshi wa
Cairo na Mohamed Barakat akaisawazishia Ahly dakika ya 62.
Ingawa hadi
sasa matokeo ya Kundi A hayajatufikia, lakini kabla ya mechi za leo Esperance ilikuwa
inaongoza kwa pointi zake 13, baada ya kucheza mechi tano, ikifuatiwa na Sunshine
Stars yenye pointi saba, wakati ES Sahel ina pointi tano katika nafasi ya tatu
na ASO Chlef haina pa kwenda ikiwa mkiani na haina pointi hata moja.
Sunshine
Stars na ES Sahel zinawania kuungana na Esperance ambayo haing’oleki tena
kileleni.
MSIMAMO WA MAKUNDI:
KUNDI A
P W D L GF GA GD Pts
1 Esperance 5 4 1 0 7 2 5 13
2 Sunshine Stars 5 2 1 2 4 4 0 7
3 ES Sahel 4 1 2 1 1 1 0 5
4 ASO Chlef 4 0 0 4 3 8 -5 0
KUNDI B
P W D L GF GA GD Pts
1 Al Ahly 6 3 2 1 9 6 3 11
2 TP Mazembe 6 3 1 2 9 6 3 10
3 Berekum Chelsea 6 2 3 1 9 10 -1 9
4 Zamalek 6 0 2 4 5 10 -5 2
No comments:
Post a Comment