Tuesday, October 2, 2012

TATIZO NI NINI KLABU YA YANGA.....MWAKA MMOJA NA NUSU MAKOCHA WANNE TOFAUTI...............

Young Africans.jpg
Jina Kamili Young Africans Sports Club
Jina la utani Yanga
Kuanzishwa 1935
Kocha; Ernest Brandts (ujerumani)








Msimu wa ligi ya Vodacom wa 2011/12 nchini Tanzania ulishuhudia Mabingwa watetezi wa Kagame cup wa wakati huo na wa sasa Yanga sports club wakiitandika Simba sports club bao moja lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa zambia Davies Mwape,ambapo ilikuwa ni mechi ya kwanza tangu mserbia Kostadin Papic aichukue timu toka kwa Sam Timbe,kocha aliyeiwezesha Yanga kutwaa kombe hilo,na vivyo hivyo kocha wa Yanga wa sasa Ernstus "Ernie" Wilhelmus Johannes Brandts atakikalia kiti hicho kwa mara ya kwanza katika pambano maarufu afrika mashariki,akichukua mikoba  kwa kocha mwenye hadhi ya juu akiwa na leseni ya ukocha toka shirikisho la soka barani ulaya'''' UEFA Pro Licence''''Tom Saintfiet ambaye wameshindwana na uongozi wa yanga na wakamsitishia mkataba wake wa miaka miwili.
Kwa hiyo ndani ya mwaka makocha tofauti wanne wamekalia kiti cha ukocha katika klabu hiyo jambo ambalo kiufundi si sahihi hasa katika nchi ambayo inashika nafasi zaidi ya 100 katika viwango vya soka duniani. 
Kwasababu sidhani kama kuna sababu ya msingi iliyotolewa na viongozi wakati hawa walimu walipokuwa wanatimuliwa,utasikia kuna wachezaji hawapendwi,mara katoa siri za ndani  ambazo hazitakiwi kutolewa ,kamtukana kiongozi mmoja wa juu  wa klabu,sababu ambazo ukikaa chini kufukiria haziingii akilini bali ni siasa ambazo zimewajaa viongozi na wale wanaojiita wazee wa timu na wale ambao husema '''sisi ndo wenye yanga na wenye uchungu nayo wakati,kadi zao za uanachama hata kulipia hawajalipia na hao ndo wananunua jezi ambazo timu haifaidiki sasa je uchungu na timu upo wapi,kwa nini huyu mshabiki mwenye uchungu asikatae kutumia kitu chenye nembo ya klabu ambacho klabu haifaidiki,ila ukija kwenye mambo kama haya ndo uchungu unakuja,bora aongee mshabiki wa ''SOFAPAKA''klabu ya majirani zetu kenya ambapo mashabiki wamenunua basi la mamilioni kwa pesa zao mfukoni,shabiki wa hii klabu akisema ana uchungu ntaelewa.
Najua kuna watu flani ndugu zangu wanazi wa yanga hasa wa pale katikati ya jiji''samora avenue''watapinga kuhusu hii nakala lakini ni ukweli lazima waulizane na kuhoji makocha wanne ndani ya mwaka inamaanisha nini katika maendeleo ya timu,mwisho wake watatoa mfano wa klabu ya chelsea nchini uingereza lakini.wale wapo katika hatua ya mbali ya soka ambapo kocha asumbuki kumfundisha mtu kuishi kiprofesheno na kuanza kumfundisha kocha alipoishia ,lakini hapa kwetu kocha akija mwingine hatoendelea alipoishia kwasababu wapi kuna ''database'' ya mipango ya mwalimu aliyeondoka,jibu halipo.hapo ndipo utakubaliana na ukweli ninaoandika,umefika wakati wa klabu zetu hapa nchini kubadilika na kuendesha timu kiufundi,na kujiuliza kunani?

No comments: