Kila nikijiangalia umri nilio nao hivi sasa najiuliza kama ningekuwa nacheza soka la kulipwa ningeweza kulinda kiwango hadi umri gani napata majibu kuwa ningestaafu nikiwa na miaka 35,na hapo ningeacha ligi ya ushindani nikiwa na 30 na miaka mitano ningeenda huko falme za kiarabu au marekani ambapo ligi si ngumu kama uingereza ambapo miaka 35 ningetangaza kustaafu huku mpira ukiwa umeisha na nguvu sina tena.
Lakini kuna mtu mmoja ambaye najiuliza ataenda falme za kiarabu lini au marekani ambapo Thierry Henry ana miaka 35 yuko marekani lakini anaonekana lulu katika ligi hiyo huku utaalamu wake umepungua kwa kiasi kikubwa,na mtu huyo ni fundi kupindukia wa mipira mirefu si mwingine ni mzaliwa wa mji wa SALFORD,GREATER MANCHESTER mwaka 1974,kaskazini magharibi mwa uingereza ''PAUL STEWART SCHOLES(37),mwanasoka aliyezaliwa katika hospitali ya''hope hospital'' ikimaanisha hospitali ya tumaini na kama ambavyo uwezo wake unakupa tumaini la kumwamini uwanjani pamoja na umri kumtupa mkono na si uwezo wake.
Kilichonishawishi kuandika nakala ni jumamosi ya tarehe 29 Septemba 2012,majira ya saa moja usiku nikiwa katikati ya jiji la dar es salaam pale mtaa wa samora ndani ya ukumbi unaoitwa''city sports lounge''nikiangalia mechi iliyovunja mwiko wa Tottenham hotspurs kutoshinda ndani ya uwanja wa old trafford tokea miaka 23 iliyopita,kuna mtu mmoja alinifanya muda wote kuamini kwamba ule mwiko hautovunjika,ni huyu paul scholes.
Alilitawala dimba vya kutosha kwa pasi fupi fupi na ndefu,hasa kipindi cha pili cha mchezo ambapo karibia kila pasi yake ilifika kwa mlengwa na kufanya old trafford kuzizima kwa makelele kila paul scholes akifanya vitu vyake,mimi na watu wengine tunashangaa tu uwezo wake tunaujadili mwisho tunaenda kupumzika majumbani kwetu.
Lakini kuna mtu ambaye afanyi hivyo anabaki kutafuta njia ya kumfanya mtu huyu amsaidie tena au anatamani mtu huyu atangaze kurudi katika soka la kimataifa hata kama hatocheza mwanzo hadi mwisho wa mchezo lakini uwepo wake katika timu ni wa muhimu sana hasa pale timu ikihitaji kukamilisha kitu flani katika wakati flani,iwe kuituliza timu baada ya kushinda kwa kumiliki mpira au kuitafutia timu ushindi kutokea katakati ya uwanja,nina kila sababu ya kusema kwamba alitakiwa kuwepo pale heatthrow,airport ya london wakati timu ikijiandaa kwenda poland na ukraine kwa ajili ya euro 2012.Huyu si mwingine bali ni kocha wa uingereza Roy Hodgson,ndio sitoshangaa siku nikiamka na kufungua tovuti ya the sun gazeti moja maarufu kule uingereza na kukuta habari kwamba''Hodgson akutwa kwenye mgahawa jijini manchester na paul scholes'',katika kizazi cha sasa cha uingereza kinachoanza na kuisha wana watu wachache ambao wanacheza mpira kwa kipaji na sio kufundishwa darasani ambao hata kupiga pasi wanataka wapige jinsi walivyofundishwa hata kama mazingira hayaruhusu,ni wachache sana kama jack wilshere.Utakapotaka timu ikae na mpira katikati basi utamuhitaji paul scholes,utakapotaka pasi ndefu za haraka utamuhitaji kiungo huyu mtukuka'' xavi hernandez aliwahi kusema hyu ni kiunga bora wa miaka 15-20,ana pasi nzuri,maono,hapotezi mipira,anavutia na kama angekuwa hispania angethaminiwa zaidi''''ila kuna kitu kimoja ambacho kinamfutia mtu huyu utakatifu wake wa soka ni faulo dhidi ya wapinzani ana rafu za hatari na za kutisha na hivyo kuwa na jumla ya kadi za njano 90 katika ligi kuu na nyekundu 4 na kadi za njano 32 katika ligi ya mabingwa na kushikilia rekodi ya kadi nyingi katika ligi ya mabingwa na nafasi ya tatu ligi kuu.
Miaka 37 bado anatawala dimba na kuwashinda wakina sandro ambao wakati yeye anacheza mpira wao ndo wanazaliwa na ndio maana sitoshtushwa ntakapomsikia mtangazaji wa kituo cha skysports''Chris kamara'' akitangaza kuwa paul scholes ni mmoja wa wachezaji watakaokuwa heathrow kuelekea katika uwanja wa ndege wa rio de janeiro nchini brazil kwenye kombe la dunia 2014,atakuwa na miaka 40 kasoro ila ninaamini anaweza akacheza hata uwepo wake kwenye benchi ni morali tosha kwa wachezaji
No comments:
Post a Comment