Tuesday, October 2, 2012

NAONA KILA DALILI YA KOCHA WA UINGEREZA ROY HODGSON KUAMKIA NYUMBANI KWA SCHOLES ALFAJIRI NA KUMUOMBA WATOKE KUPATA CHAI KATIKA MGAHAWA MMOJA WA JIJI LA MANCHESTER....................................

Kila nikijiangalia umri nilio nao hivi sasa najiuliza kama ningekuwa nacheza soka la kulipwa ningeweza kulinda kiwango hadi umri gani napata majibu kuwa ningestaafu nikiwa na miaka 35,na hapo ningeacha ligi ya ushindani nikiwa na 30 na miaka mitano ningeenda huko falme za kiarabu au marekani ambapo ligi si ngumu kama uingereza ambapo miaka 35 ningetangaza kustaafu huku mpira ukiwa umeisha na nguvu sina tena.
Lakini kuna mtu mmoja ambaye najiuliza ataenda falme za kiarabu lini au marekani ambapo Thierry Henry ana miaka 35 yuko marekani  lakini anaonekana lulu katika ligi hiyo huku utaalamu wake umepungua kwa kiasi kikubwa,na mtu huyo ni fundi kupindukia wa mipira mirefu si mwingine ni mzaliwa wa mji wa SALFORD,GREATER MANCHESTER mwaka 1974,kaskazini magharibi mwa uingereza ''PAUL STEWART SCHOLES(37),mwanasoka aliyezaliwa katika hospitali ya''hope hospital'' ikimaanisha hospitali ya tumaini  na kama ambavyo uwezo wake unakupa tumaini la kumwamini uwanjani pamoja na umri kumtupa mkono na si uwezo  wake.
Kilichonishawishi kuandika nakala ni jumamosi ya tarehe 29 Septemba 2012,majira ya saa moja usiku nikiwa katikati ya jiji la dar es salaam pale mtaa wa samora ndani ya ukumbi unaoitwa''city sports lounge''nikiangalia mechi iliyovunja mwiko wa Tottenham hotspurs kutoshinda ndani ya uwanja wa old trafford tokea miaka 23 iliyopita,kuna mtu mmoja alinifanya muda wote kuamini kwamba ule mwiko hautovunjika,ni huyu paul scholes.
Alilitawala dimba vya kutosha kwa pasi fupi fupi na ndefu,hasa kipindi cha pili cha mchezo ambapo karibia kila pasi yake ilifika kwa mlengwa na kufanya old trafford kuzizima kwa makelele kila paul scholes akifanya vitu vyake,mimi na watu wengine tunashangaa tu uwezo wake tunaujadili mwisho tunaenda kupumzika majumbani kwetu.
Lakini kuna mtu ambaye afanyi hivyo anabaki kutafuta njia ya kumfanya mtu huyu amsaidie tena au anatamani mtu huyu atangaze kurudi katika soka la kimataifa hata kama hatocheza mwanzo hadi mwisho wa mchezo lakini uwepo wake katika timu ni wa muhimu sana hasa pale timu ikihitaji kukamilisha kitu flani katika wakati flani,iwe kuituliza timu baada ya kushinda kwa kumiliki mpira au kuitafutia timu ushindi kutokea katakati ya uwanja,nina kila sababu ya kusema kwamba alitakiwa kuwepo pale heatthrow,airport ya london wakati timu ikijiandaa kwenda poland na ukraine kwa ajili ya euro 2012.Huyu si mwingine bali ni kocha wa uingereza Roy Hodgson,ndio sitoshangaa siku nikiamka na kufungua tovuti ya the sun gazeti moja maarufu kule uingereza na kukuta habari kwamba''Hodgson akutwa kwenye mgahawa jijini manchester na paul scholes'',katika kizazi cha sasa cha uingereza kinachoanza na kuisha wana watu wachache ambao wanacheza mpira kwa kipaji na sio kufundishwa darasani ambao hata kupiga pasi wanataka wapige jinsi walivyofundishwa hata kama mazingira hayaruhusu,ni wachache sana kama jack wilshere.Utakapotaka timu ikae na mpira katikati basi utamuhitaji paul scholes,utakapotaka pasi ndefu za haraka utamuhitaji kiungo huyu mtukuka'' xavi hernandez aliwahi kusema hyu ni kiunga bora wa miaka 15-20,ana pasi nzuri,maono,hapotezi mipira,anavutia na kama angekuwa hispania angethaminiwa zaidi''''ila kuna kitu kimoja ambacho kinamfutia mtu huyu utakatifu wake wa soka ni faulo dhidi ya wapinzani ana rafu za hatari na za  kutisha na hivyo kuwa na jumla ya kadi za njano 90 katika ligi kuu  na nyekundu 4 na kadi za njano 32 katika ligi ya mabingwa na kushikilia rekodi ya kadi nyingi katika ligi ya mabingwa na  nafasi ya tatu ligi kuu.
Miaka 37 bado anatawala dimba na kuwashinda wakina sandro ambao wakati yeye anacheza mpira wao ndo wanazaliwa na ndio maana sitoshtushwa ntakapomsikia mtangazaji wa kituo cha skysports''Chris kamara'' akitangaza kuwa paul scholes ni mmoja wa wachezaji watakaokuwa heathrow kuelekea katika uwanja wa ndege wa rio de janeiro nchini brazil kwenye kombe la dunia 2014,atakuwa na miaka 40 kasoro ila ninaamini anaweza akacheza hata uwepo wake kwenye benchi ni morali tosha kwa wachezaji

TATIZO NI NINI KLABU YA YANGA.....MWAKA MMOJA NA NUSU MAKOCHA WANNE TOFAUTI...............

Young Africans.jpg
Jina Kamili Young Africans Sports Club
Jina la utani Yanga
Kuanzishwa 1935
Kocha; Ernest Brandts (ujerumani)








Msimu wa ligi ya Vodacom wa 2011/12 nchini Tanzania ulishuhudia Mabingwa watetezi wa Kagame cup wa wakati huo na wa sasa Yanga sports club wakiitandika Simba sports club bao moja lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa zambia Davies Mwape,ambapo ilikuwa ni mechi ya kwanza tangu mserbia Kostadin Papic aichukue timu toka kwa Sam Timbe,kocha aliyeiwezesha Yanga kutwaa kombe hilo,na vivyo hivyo kocha wa Yanga wa sasa Ernstus "Ernie" Wilhelmus Johannes Brandts atakikalia kiti hicho kwa mara ya kwanza katika pambano maarufu afrika mashariki,akichukua mikoba  kwa kocha mwenye hadhi ya juu akiwa na leseni ya ukocha toka shirikisho la soka barani ulaya'''' UEFA Pro Licence''''Tom Saintfiet ambaye wameshindwana na uongozi wa yanga na wakamsitishia mkataba wake wa miaka miwili.
Kwa hiyo ndani ya mwaka makocha tofauti wanne wamekalia kiti cha ukocha katika klabu hiyo jambo ambalo kiufundi si sahihi hasa katika nchi ambayo inashika nafasi zaidi ya 100 katika viwango vya soka duniani. 
Kwasababu sidhani kama kuna sababu ya msingi iliyotolewa na viongozi wakati hawa walimu walipokuwa wanatimuliwa,utasikia kuna wachezaji hawapendwi,mara katoa siri za ndani  ambazo hazitakiwi kutolewa ,kamtukana kiongozi mmoja wa juu  wa klabu,sababu ambazo ukikaa chini kufukiria haziingii akilini bali ni siasa ambazo zimewajaa viongozi na wale wanaojiita wazee wa timu na wale ambao husema '''sisi ndo wenye yanga na wenye uchungu nayo wakati,kadi zao za uanachama hata kulipia hawajalipia na hao ndo wananunua jezi ambazo timu haifaidiki sasa je uchungu na timu upo wapi,kwa nini huyu mshabiki mwenye uchungu asikatae kutumia kitu chenye nembo ya klabu ambacho klabu haifaidiki,ila ukija kwenye mambo kama haya ndo uchungu unakuja,bora aongee mshabiki wa ''SOFAPAKA''klabu ya majirani zetu kenya ambapo mashabiki wamenunua basi la mamilioni kwa pesa zao mfukoni,shabiki wa hii klabu akisema ana uchungu ntaelewa.
Najua kuna watu flani ndugu zangu wanazi wa yanga hasa wa pale katikati ya jiji''samora avenue''watapinga kuhusu hii nakala lakini ni ukweli lazima waulizane na kuhoji makocha wanne ndani ya mwaka inamaanisha nini katika maendeleo ya timu,mwisho wake watatoa mfano wa klabu ya chelsea nchini uingereza lakini.wale wapo katika hatua ya mbali ya soka ambapo kocha asumbuki kumfundisha mtu kuishi kiprofesheno na kuanza kumfundisha kocha alipoishia ,lakini hapa kwetu kocha akija mwingine hatoendelea alipoishia kwasababu wapi kuna ''database'' ya mipango ya mwalimu aliyeondoka,jibu halipo.hapo ndipo utakubaliana na ukweli ninaoandika,umefika wakati wa klabu zetu hapa nchini kubadilika na kuendesha timu kiufundi,na kujiuliza kunani?

Kumekucha ligi ya mabingwa barani ulaya.....viwanja 8 kuwaka moto...............

MudaHome AwayKundiUwanaja
09:45 EAT FC Nordsjælland  v  Chelsea Group E Farum Park
09:45 EAT Juventus  v  Shakhtar Donetsk Group E Juventus Stadium
09:45 EAT BATE Borisov  v  Bayern Munich Group F Dynamo Stadium, Minsk
09:45 EAT Valencia  v  Lille Group F Estadio Mestalla
07:00 EAT Spartak Moscow  v  Celtic Group G Luzhniki Stadium
09:45 EAT Benfica  v  Barcelona Group G Estadio da Luz
09:45 EAT CFR Cluj-Napoca  v  Manchester United Group H Stadionul Dr. Constantin Radulescu
09:45 EAT Galatasaray  v  Braga Group H Türk Telekom Arena

Friday, September 28, 2012

ITS THE LONDON DERBY AGAIN,ARSENAL VS CHELSEA LOCK HORNS AGAIN AT EMIRATES STADIUM TOMORROW.............LETS DIG INTO THEIR RIVARLY.......

Arsenal F.C.–Chelsea F.C. rivalry

Background

While they never considered each other primary rivals, as two of the top clubs in London there has always been strong needle between the fans dating back to the 1930s. Matches between them would often attract large attendances. The Arsenal and Chelsea rivalry has been more recently considered an important derby, after Chelsea's rise to the top class of the Premier League in 2000s, when the two started to compete constantly for the English championship. According to an internet survey of fans in December 2003, the Arsenal fans who responded to the survey said that they considered Chelsea as their third rival, after Manchester United and Tottenham Hotspur.[1] Those Chelsea fans who responded to the survey said that they considered Arsenal as their main rival, however Tottenham and Fulham are their more traditional rivals.[1] In a 2009 survey by the Football Fans Census, Arsenal fans named Chelsea as the club they disliked the most, ahead of their traditional rivals Tottenham. Chelsea fans named Arsenal as their second most-disliked club, behind Liverpool.[2]

History

The first league meeting between the two teams took place on November 9, 1907 at Stamford Bridge. This was the first Football League First Division game played between two London clubs and drew a then First Division record crowd of 65,000. A match between the clubs at Stamford Bridge in 1935 drew a crowd of 82,905, the second highest recorded attendance for an English league match. They met in two close contested FA Cup semi-finals in the 1950s, with Arsenal winning both times. In the 1960s Chelsea dominated the tie with 14 wins, two draws and just 2 losses during the decade.[3]
More recently the clubs have contested two major finals, the 2002 FA Cup Final, which Arsenal won 2–0, and the 2007 Football League Cup Final, which Chelsea won 2–1. The two teams have also met in the UEFA Champions League in the quarter-finals in 2003–04 drawing 1–1 at Stamford Bridge, and Chelsea winning 2–1 at Highbury to go through to the semi-finals.
In 2006 the transfer of Ashley Cole from Arsenal to Chelsea further stoked the rivalry, as Cole had been caught meeting Chelsea officials months before.[4]
The 2007 Carling Cup final was one of the most noted incidents. The game was marred by a fracas involving Frank Lampard, Cesc Fàbregas and others that resulted in yellow cards for the two and three other players sent off, the supposed wrongful dismissal of Emmanuel Adebayor and incidents of Chelsea fans throwing celery at Arsenal players. This led the media to dub it the "Snarling Cup final".
On December 27, 2010, Chelsea came into the Emirates having beaten Arsenal 5 times in a row by a goal differencial of 13–2. Arsenal were victorious upon the final whistle however by a score of 3–1.
On 29 October 2011, another thrilling and fantastic game was played at Stamford Bridge. Arsenal won 5–3 with Robin Van Persie scoring a hat-trick and André Santos and Theo Walcott scoring one goal each. Frank Lampard, John Terry and Juan Mata scored the goals for Chelsea[5]
Overall, Arsenal have won the more games in history, having won 70 times to Chelsea's 54, with 52 draws (as of 21 April 2012).[6] Arsenal's record win was a 5–1 victory in a First Division match at Stamford Bridge on November 29, 1930. Chelsea's record win was a 5–0 victory at Highbury in the League Cup on November 11, 1998.
Former Chelsea Striker Didier Drogba holds the mark for the most derby goals with 13.

Tuesday, September 25, 2012

Chelsea yatoa kipigo cha mbwa mwizi kwa wolves............

Chelsea imeingia duru la nne la kombe la ligi kwa kishindo kwa kuishindilia wolves magoli 6-0,katika dimba la stamford bridge,magoli ya romeu,ryan bertrand,juan mata,torres,cahill na goli la kwanza la victor mosses tangu avae uzi wa ''the blues'' yalitosha kuwapa matajiri wa london ushindi mnono.

Asto Villa yazima ndoto za majirani wa man united na kufuzu duru la nne la kombe la ligi................

. Aston Villa imeushtua ulimwengu katika kile kisichotegemewa na wengi kwa kuichapa man city 4-2 baada ya muda wa ziada,na kufuzu duru la nne la capital one cup,na isitoshe katika uwanja wao wa etihad. Villa ilibidi watoke nyuma mara mbili kabala ya gabriel agbonlahor na Charles N'Zogbia kuipa ushindi villa baada ya muda wa ziada. City walikuwa wa kwanza kuongoza kupitia Mtukutu Balloteli baada ya kazi nzuri ya James Milner,lakini goli la kujifunga la Barry liliwafanya wawiane. Shuti la umbali la wa yadi 20 la Kolarov liliwapa city ahueni kabla ya Agbonlahor kuisawazishia dakika tano baada ya city kuongoza,na mechi kuendelea katika muda wa ziada ambapo Agbonlahor na N'zogbia waliizamisha city. Mancini aliweka nyuso mpya kumi kasoro lescott aliyeingia baada ya Jack Rodwell kuumia wakati wa kupasha misuli.